PROGRAMU YA SIMU YA PLANTVILLAGE

Posted on March 11, 2021 by PlantVillage

 

PlantVillage Nuru ni Nini?

 • Nuru ni akili bandia katika utambuzi wa magonjwa na wadudu wanaoshambulia mazao.
 • Nuru ina uwezo wa kutambua uwepo wa magonjwa kwa kuangalia dalili zinazoonekana katika majani.
 • Programu ya Nuru ina uwezo wa kutambua magonjwa ya michirizi kahawia,batobato na athari za tanabui katika mihogo. Pia inaweza kutambua athari zinazoletwa na viwavi jeshi katika mahindi.

Faida za programu ya Nuru

 • Ina uwezo wa kufanya uchunguzi na kutoa matokeo papo kwa hapo.
 • Inakupea ushauri wa namna ya kuyadhibiti magonjwa iliyotambua.
 • Inakuunganisha na wataalamu wa kilimo na watumiaji wengine walioko sehemu mbalimbali.
 • Inatoa taarifa za kukuwezesha kujifunza kuhusu mimea mbalimbali.
 • Inaweza kutumika bila kuingia katika mtandao.
 • Inatumia lugha mbalimbali kama Kiswahili,Kingereza n.k

Hatua ya kupakua Nuru kwenye simu yako

 1. Fungua Google Play Store
 2. Andika PlantVillage Nuru
 3. Bonyeza kitufe cha pakua
 4. Fungua Programu ya PlantVillage Nuru
 5. Programu ya Nuru itaomba ruhusa ya kutumia kamera ya simu yako na kukuelekeza kwenye usajili

 

Kiunga cha kupakua:http://play.google.com/store/apps/details?id=plantvillage.nuru

 

Imeandikwa na Mercyline Tata

 

 


 


 


 


 


 


 


 
PlantVillage PlantVillage logo